Baraza la OUT lasisitiza mabadiliko kwa vitendo

DAR-Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Bi Mercy Sila, ametoa wito kwa OUT kupitia Manejimenti yake kufanya kazi kwa bidii ili kuonyesha mabadiliko kwa vitendo.
Bi. Sila, ameyasema hayo wakati akiwakaribisha wajumbe wapya wa Baraza hilo na kuwaaga wanaomaliza muda wao katika kikao cha 120 cha Baraza hilo kilichofanyika Juni 27, 2024 makao makuu ya chuo hiki, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Akiongea katika Baraza hilo amewataka wajumbe wapya ambao pia ni sehemu ya Menejimenti mpya ya chuo kuhakikisha kuwa Baraza linashuhudia utendaji uliotukuka kwa kuwatumia wataalam iliyonao ili kuleta uwajibikaji hasa katika uwekezaji na huduma za kitaalam kwa lengo la kuinua mapato na sifa ya chuo hiki.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ambaye pia ni mjumbe wa Baraza hilo, Prof. Elifas Bisanda, amewataka wajumbe hao wapya kuzingatia weledi katika ufanyaji wa kazi na kuwa kiungo imara cha uhusiano mzuri kazini baina ya watumishi na Menejimenti ili ifikapo vikao vya Baraza waweze kuonyesha mafanikio halisi.
Naye Mwanasheria wa Chuo na Katibu wa Baraza hilo, Wakili Nelly Moshi, amewataka wajumbe wapya wa Baraza hilo kuzingatia dira na uelekeo wa chuo ili kukipeleka chuo katika malengo iliyojipangia kwa wakati na ufanisi mkubwa.

Baraza la Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, ndiyo chombo cha juu chenye maamuzi ya mwisho ambapo Baraza hilo limeketi kikao chake cha 120, Juni 27, 2024 na kushuhudia wajumbe wapya waliopokelewa katika kikao hiki ambao ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia Taaluma, Tafiti na Huduma za Ushauri wa Kitaalam, Prof. Alex Makulilo.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo anayeshughulika na Mipango, Fedha na Utawala, Prof. Josiah Katani na Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa chuo anayesimamia Huduma za Mikoa na Teknolojia za Kujifunzia, Prof. Leonard Fweja.

Aidha, baraza limemuaga Prof. Ndelilio Urio, aliyemaliza muda wake kama mjumbe wa Baraza hilo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news