BoT kutoa miongozo ya kukomesha mikopo umiza

DAR-Benki Kuu ya Tanzania (BoT) iko mbioni kutoa kanuni mpya zinazoainisha miongozo na utaratibu wa kufuatwa katika Uendeshaji wa Huduma Ndogo za Fedha kwa Daraja la Pili ili kukabiliana na changamoto zilizopo ikiwemo gharama za juu za mikopo, uvunjifu wa sheria na kutokuzingatia utu katika utoaji wa mikopo.Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya awamu ya kwanza kwa watoa huduma ndogo za fedha, Gavana wa BoT, Bw. Emmanuel Tutuba, amesema Benki Kuu imekuwa ikipokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kutokana na kukithiri kwa vitendo vya kutoa mikopo na kudai madeni kinyume cha utaratibu.

“Tumesikia mara nyingi wananchi wakilalamika kunadaiwa mali zao bila kufuata utaratibu, kushikilia kadi zao za benki (ATM), mikopo mingi yenye gharama kubwa zisizoeleweka, kuwekwa ndani pindi wasipolipa kwa wakati. Hili si jambo zuri la kufumbia macho hata kidogo,” amesema Gavana Tutuba.

Amesema, ili kukabiliana na changamoto hizo BoT, imeamua kuja na kanuni zitakazosaidia kuondoa kero hizo katika sekta hiyo.

“Tumetengeneza kanuni ambazo zitatoka mwezi Julai mwaka huu 2024, zikiainisha miongozo na taratibu za kufuatwa katika uendeshaji wa huduma ndogo za fedha kwa Daraja la Pili ikiwa ni pamoja na adhabu kwa wanaokiuka sheria,” ameeleza.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Bw. Sadati Musa, amesema kwa kushirikiana na Chuo cha Benki Kuu, tayari mafunzo yametolewa kwa watoa huduma ndogo za fedha zaidi ya 1,000 nchini ili kupunguza na kuondoa changamoto zilizopo katika utoaji wa mikopo.

Nao baadhi ya watoa huduma ndogo za fedha, wamesema mafunzo hayo yatawasadia kutoa huduma za mikopo kwa weledi na kwa kuzingatia miongozo mbalimbali ya Serikali huku wakiwahimiza wananchi kupata elimu ya fedha ili kuondoa changamoto na misuguano inayojitokeza mara kwa mara.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news