DODOMA-Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamepitisha kwa kishindo Bajeti Kuu ya Serikali ya shilingi trilioni 49.35 kwa mwaka 2024/25, bungeni jijini Dodoma, ambapo katika zoezi la upigaji kura, Wabunge 362 wamepiga kura za ndio na wabunge 18 wamepiga kura za kutoamua.