Bunge lapitisha kwa kishindo Bajeti ya Wizara ya Fedha shilingi trilioni 18.17, viongozi wapongeza

DODOMA-Matukio Mbalimbali ya Viongozi wa Wizara ya Fedha na Taasisi zake wakiwapongeza Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb) na Naibu Waziri wake, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitisha kwa kishindo Makadirio ya Mapato na Matumizi (Bajeti) ya Wizara ya Fedha ya shilingi trilioni 18.17 kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025.
Kati ya Fedha hizo, shilingi trilioni 17.63 ni matumizi ya kawaida yakihusisha kulipa deni la Serikali shilingi trilioni 13.13; shilingi bilioni 946.45 za mishahara; matumizi mengineyo ni shilingi bilioni 937.30; huduma za Mfuko Mkuu wa Serikali shilingi trilioni 2.61; na matumizi ya Maendeleo ni shilingi bilioni 544.05.
Vilevile Bunge hilo limeidhinisha mapato ya Fungu 045 ambayo ni matumizi ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (CAG), kiasi cha shilingi bilioni 112.73 ambapo kiasi cha shilingi bilioni 101.26 ni matumizi ya kawaida na shilingi bilioni 11.47 ni matumizi ya maendeleo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news