BVR Kits 6,000 kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura

DAR-Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imekamilisha maandalizi muhimu kwa ajili ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ikiwa ni pamoja na ununuzi wa vifaa vya uandikishaji vinavyojumuisha BVR Kits 6,000.Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele akiendesha majadiliano wakati wa mkutano wa tume na viongozi wa dini unaofanyika leo Juni 10, 2024 mkoani Dar es Salaam.

Hayo yamebainishwa leo Juni 10, 2024 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw.Ramadhani Kailima wakati akiwasilisha mada kwenye mkutano wa tume na viongozi wa dini.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa tume na viongozi wa dini uliofanyika leo Juni 10, 2024 mkoani Dar es Salaam.

Mkutano huo umefanyika sambamba na mkutano wa Tume na Taasisi na Asasi za Kiraia ikiwa ni muendelezo wa utaratibu wa tume wa kuwashirikisha wadau wa uchaguzi kabla ya kuanza rasmi kwa uboreshaji wa daftari.
Baadhi ya viongozi wa dini waliohudhuria mkutano huo wakifuatilia mada.
Mada ya uboreshaji ikifanyika kwa vitendo.

Bw. Kailima amesema, BVR Kits hizo zitatumia vishikwambi kuchukua taarifa za wapiga kura ikiwemo picha, saini na alama za vidole.

“BVR Kits za sasa zinatumia mfumo endeshi wa android na uzito wake ni kilogramu 18, awali zilikuwa zinatumia mfumo endeshi wa window na uzito wa kilogramu 35," amesema Bw. Kailima. Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima akiwasilisha mada kwenye mkutano wa tume na  viongozi wa dini.

Amesema, Mfumo wa Uandikishaji wa Wapiga Kura (Voters Registration System-VRS) umefanyiwa usanifu na kuboreshwa ili kukidhi aina ya BVR Kits za sasa ambazo zinatumia programu endeshi ya android.

Wakati akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele amesema, BRV Kits hizo zitakuwa rahisi kubeba na kufanya zoezi la uboreshaji wa Daftari kuwa rahisi haswa kwenye maeneo ya vijijini ambapo watendaji hulazimika kubeba vifaa kwa umbali mrefu.Baadhi ya viongozi wa dini waliohudhuria mkutano huo wakifuatilia mada.

Amesema, mfumo wa teknolojia hii ya BVR hutumika katika kumtambua mtu na kumtofautisha na mwingine. Uandikishaji huu wa wapiga kura utahusisha uchukuaji wa alama za vidole vya mikono, picha na saini na kuhifadhiwa kwenye kanzidata ya wapiga kura, amesema.
Baadhi ya viongozi wa dini waliohudhuria mkutano huo wakifuatilia mada.

Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utazinduliwa mkoani Kigoma tarehe 01 Julai, 2024 na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news