CCM yasisitiza umuhimu wa kukuza sekta binafsi na uwekezaji

TANGA-Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kwamba hakutakuwa na mabadiliko ya kweli katika kukuza uchumi wa nchi, endapo sekta binafsi hazitapewa kipaumbele katika uwekezaji nchini.
Hayo yamesemwa leo Juni 8, 2024 jijini Tanga na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi alipokuwa akizindua Kiwanda cha kuzalisha nyaya za umeme na kupeleka umeme Vijijini cha Tanga Cable kilichopo mkoani Tanga.
"Hatakuwa na mabadiliko ya kweli katika kukuza uchumi wa nchi, endapo Sekta binafsi hazitapewa kipaumbele katika uwekezaji nchini.Serikali ya CCM itaendelea kusimamia sera yake ya kuhakikisha uwekezaji unafanyika nchini, ili kuweza kukuza uchumi wa nchi.

"Kwani ndiyo Ilani ya CCM inavyosema katika upande ufufuaji wa viwanda vilivyokufa na kuanzisha vipya.Napongeza za uongozi wa Tanga Cable kwa hatua hii nzuri mliyochukua ya kuhakikisha mnawekeza nchini,"amesema .

Ameongeza kwamba hatua hiyo inakwenda hivyo kuongeza kupanda kwa uchumi nchini na kutoa mwito kwa taasisi za kiserikali,sekta binafsi na wananchi kujenga utamaduni wa kutumia bidhaa za ndani baada ya kujiridhisha ubora wake, ili kuwezesha viwanda kukua kiuchumi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tanga Cable, Murtaza Dossaji, amesema Tanga Cable ni miongoni mwa viwanda bora nchini, ambapo pia kinaenda kutoa ajira kwa zaidi ya watu 50.
Ameongeza kuwa, nia ya kiwanda hicho ni kuboresha sekta ya nishati ya umeme nchini huku akifafanua kiwanda hicho kimekuwepo kwa takribani zaidi ya miaka 60 nchini Tanzania na uwekezaji wake ukiwa ni zaidi ya shilingi bilioni moja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news