DC Machali azindua jengo la Dawati la Jinsia na Watoto wilayani Mkalama

SINGIDA-Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Moses Machali amezindua jengo la Dawati la Jinsia na Watoto linalopatikana katika Kituo kikuu cha polisi wilayani Mkalama ikiwa ni jihudi za serikali katika kutokomeza ukatili wa kijinsia nchini Tanzania.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo hilo Juni 29,2024 amewataka wakazi wilayani Mkalama kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia wilayani Mkalama.
“Kila mmoja ahakikishe anapambana kutoa taarifa kuhusu ukatili wa kijinsia kwenye mamlaka zinazohusika, tutumie Jeshi letu la polisi vizuri. Sisi sote tunapaswa kuwa mashujaa katika mapambano haya."

Aidha, Mhe. Moses Machali amewasisitiza wazazi Wilayani Mkalama kuwapeleka watoto wao shule ili waweze kutimiza ndoto zao za kimaisha na mzazi atakayekataa kumpeleka mtoto shule serikali itamchukulia hatua kali dhidi yake.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamishina wa KKamisheni ya Polisi Jamii, CP Faustine Shilogile, amesema vitendo vya ukatili vimeongezeka nchini kwa mwaka 2023 kulinganisha na mwaka 2022 huku moja ya sababu ya kuongezeka kwa vitendo hivyo ni kutokana na uelewa mkubwa wa jamii katika kuripoti matukio ya ukatili kulinganisha na miaka ya nyuma.
“Kwa mwaka 2023 vitendo vya ukatili viliongezeka hadi kufikia 22,147 kulinganisha na matukio 18,403 kwa mwaka 2022 kwa watu wazima na kwa upande wa watoto matukio yaliyoriptiwa ni 15,301 kulinganisha na 12,162 kwa mwaka 2022."
Naye Naibu Mwakilishi Mkazi UNWOMEN, Katherine Gifford amelipongeza Jeshi la Polisi nchini Tanzania na serikali kwa ujumla kwa kuwa mstari wa mbele katika kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news