Dkt.Biteko aiagiza TANESCO kujenga laini mpya ya umeme Ushirombo

GEITA-Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe.Dkt Doto Biteko ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kujenga laini mpya ya Umeme kutoka Nyakanazi-Ushirombo na Kahama Bongwe hadi Bukombe ili kuhakikisha hali ya upatikanaji wa umeme katika Wilaya ya Bukombe inaimarika.
Dkt.Biteko ametoa agizo hilo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Jimbo la Bukombe, Mkoa wa Geita ambapo amesema kuwa sambamba na ujenzi wa laini hizo za umeme, kutajengwa kituo cha kupoza Umeme Bukombe ili kuhakikisha wananchi wakiwemo wa Ushirombo wilayani Bukombe wananufaika na umeme wa uhakika.
‘’Umeme tunaopata Bukombe unatoka Bulyanhulu, unapita Mbogwe na kuja Bukombe ambapo ukifika hapa unakuwa na nguvu hafifu na ikitokea hitilafu Bulyanhulu Bukombe pia inakosa umeme hivyo ni vema TANESCO ikajenga laini hizo mpya ili wananchi wa Bukombe wapate umeme wa uhakika,"amesema Mhe.Biteko.
Kuhusu uwepo wa umeme wa kutosha nchini, Dkt. Biteko amesema Serikali imefanya kazi kubwa ya kuhakikisha wanaondoa mgao wa umeme kwa kuongeza vyanzo mbalimbali vya uzalishaji umeme na hivyo kuondoa tatizo la kukatika mara kwa mara kwa nishati hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news