Dkt.Biteko akutana na wawekezaji wa Modern Industrial Park

DODOMA-Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amekutana na kufanya mazungumzo na wawekezaji wa Modern Industrial Park wanaomiliki kongani ya viwanda eneo la Kibaha mkoani Pwani.
Mazungumzo hayo yamefanyika leo tarehe 24 Juni, 2024 katika ofisi za Naibu Waziri Mkuu Bungeni jijini Dodoma.
Aidha, Dkt. Biteko amewaeleza wawekezaji hao kuwa Serikali iko tayari kushirikiana nao na kuwapatia umeme kwa ajili ya kuwezesha shughuli za uwekezaji katika eneo hilo.
Naye, mwakilishi wa kampuni ya Modern Industrial Park, Bw. Yusuf Manzi alisema kuwa eneo hilo lina uwezo wa kubeba viwanda 202 vya aina mbalimbali na tayari miundombinu wezeshi kama maji, Ulinzi na usalama pamoja na barabara vimeshawekwa kwa ajili ya kurahisisha uwekezaji katika eneo hilo ambalo lina uhitaji wa 200MW za umeme kwa ajili ya kutumika na wawekezaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news