Dkt.Msonde awataka walimu kufundisha Kiingereza kwa umahiri

NA JAMES MWANAMYOTO
OR-TAMISEMI

NAIBU Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Elimu),Dkt. Charles Msonde amewataka walimu wa shule za sekondari nchini kufundisha wanafunzi lugha ya Kiingereza kwa umahiri ili kuwawezesha kupata ufaulu mzuri katika masomo yote ya mtihani wa kidato cha nne, ikizingatiwa kuwa Kiingereza ndio lugha rasmi ya kufundishia.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Elimu) Dkt. Charles Msonde akicheza ngoma ya asili na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Bugene Wilayani Karagwe, alipoitembelea shule hiyo ili kukagua miundombinu inayojengwa.

Dkt. Msonde ametoa wito huo kwa walimu wote wa sekondari nchini, wakati wa vikao kazi vyake na Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa Shule, Walimu Wakuu na Walimu waliopo katika Halmashauri za Wilaya ya Misenyi na Karagwe.
Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa Shule, Walimu Wakuu na Walimu waliopo Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Elimu) Dkt. Charles Msonde wakati wa kikao kazi chao na Naibu Katibu Mkuu huyo.
Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa Shule, Walimu Wakuu na Walimu waliopo Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Elimu) Dkt. Charles Msonde wakati wa kikao kazi chao na Naibu Katibu Mkuu huyo.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Elimu) Dkt. Charles Msonde akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Bugene Wilayani Karagwe (hawapo pichani) alipoitembelea shule hiyo ili kukagua miundombinu inayojengwa katika shule hiyo.

“Walimu zingatieni kufundisha kiingereza kwani wanafunzi wakiwa na umahiri wa kuongea, kusoma na kuandika lugha ya kiingereza watapa ufaulu mzuri katika mtihani wa kidato cha nne, na hakutakuwa na divisheni ziro,” Dkt. Msonde amesisitiza.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Bugene Wilayani Karagwe wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Elimu) Dkt. Charles Msonde (hayupo pichani) alipoitembelea shule hiyo ili kukagua miundombinu inayojengwa.

Dkt. Msonde amesema, hivisasa walimu wanapaswa kuwa vitani katika kuleta mapinduzi ya elimu nchini hivyo ufundishaji wa mazoea hauna nafasi katika kipindi hiki cha utawala wa Serikali ya Awamu ya Sita ambayo ina dhamira ya dhati ya kuboresha elimu kwa masilahi na manufaa ya taifa.

“Haiwezekani mtoto afundishwe na mwalimu kiingereza mwaka mzima alafu ashindwe hata kutamka neno la kiingereza uncle, kamwe haiwezekani na ndio maana walimu mnapaswa kuingia vitani ili kutatua changamoto hii ya lugha ya Kiingereza,” Dkt. Msonde amesisitiza.Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Elimu), Dkt. Charles Msonde akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Bugene Wilayani Karagwe walioonesha umahiri wa kuzungumza kiingereza, alipoitembelea shule hiyo ili kukagua miundombinu inayojengwa.

Dkt. Msonde ameongeza kuwa, katika elimu ya Sekondari lugha rasmi ya kufundishia ni kiingereza hivyo walimu wanapaswa kuitumia lugha hiyo kuwafundisha watoto mpaka waelewe, kwani mkakati wa kuboresha elimu umemlenga mtoto ili apate ujuzi kama ulivyoanishwa kwenye mtaala.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Elimu) Dkt. Charles Msonde akisikiliza umahiri wa kuongea Kiingereza wa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Bugene, alipoitembelea shule hiyo ili kukagua miundombinu inayojengwa.

Dkt. Msonde amehitimisha siku ya tatu ya ziara yake mkoani Kagera kwa kufanya vikao kazi na Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa Shule, Walimu Wakuu na Walimu waliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi na Karagwe ambapo amehimiza uwajibikaji kwa maafisa hao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news