Dkt.Nchimbi ahitimisha ziara ya kishindo Arusha

ARUSHA-Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akizungumza na wananchi wa eneo la Usa River Wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha aliposimama kuwasalimia akiwa njiani kutokea Arusha Mjini akihitimisha ziara ya siku tatu mkoani humo, kisha kuelekea Mji wa Bomang’ombe, Wilaya ya Hai, tayari kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani Kilimanjaro.
Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu Balozi Nchimbi ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Komredi Amos Gabriel Makalla na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Rabia Hamid Abdalla.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news