EWURA yatangaza bei mpya ya mafuta leo, tazama hapa

NA GODFREY NNKO

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya Petroli hapa nchini zitakazotumika kuanzia leo Juni 5, 2024.

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt.James Andilile amesema kuwa,kwa mwezi Juni mwaka huu, bei kikomo za rejareja kwa lita ya Petroli kwa Bandari ya Dar es Salaam ni shilingi 3,261 huku Tanga ikiwa shilingi 3,263 kwa lita.

Kwa upande wa Bandari ya Mtwara lita ya Petroli kwa rejareja ni shilingi 3,267. Aidha, bei kikomo ya lita ya Diezel kwa Bandari ya Dar es Salaam ni shilingi 3,112, Bandari ya Tanga shilingi 3,121 na Mtwara ni shilingi 3,122.

Mafuta ya taa, bei kikomo kwa lita katika Bandari ya Dar es Salaam ni shilingi 3,261 huku kwa upande wa Bandari ya Tanga lita moja ikiwa ni shilingi 3,307 na Mtwara ikiwa ni shilingi 3,333.

Kwa upande wa bei za jumla, bei kikomo kwa lita ya Petroli katika Bandari ya Dar es Salaam ni shilingi 3,128.72 huku kwa Bandari ya Tanga lita ikiwa ni shilingi 3,131.14 na Mtwara shilingi 3,134.43.

Aidha, kwa upande wa Diezel bei ya jumla kwa lita katika Bandari ya Dar res Salaam ni shilingi 2,979.99 huku Bandari ya Tanga lita ikiwa ni shilingi 2,988.78 na Bandari ya Mtwara lita ikiwa ni shilingi 2,989.84.Na bei kikomo ya mafuta ya taa ya jumla kwa lita katika Bandari ya Dar es Salaam ni shilingi 3,128.69.

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt.James Andilile amesema, mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Juni, 2024 yamechangiwa na kupungua kwa bei za mafuta yaliyosafishwa katika Soko la Dunia (FOB) kwa wastani wa asilimia 11.82 kwa mafuta ya petroli.

Vilevile kwa asilimia 7.77 kwa mafuta ya dizeli na asilimia 7.94 kwa mafuta ya taa, pia kuongezeka kwa wastani wa gharama za kubadilisha fedha za kigeni (Applicable Exchange Rate) kwa asilimia 1.4.

Jambo lingine ni kupungua kwa gharama za uagizaji wa mafuta (premiums) kwa wastani wa asilimia 2.06 kwa petroli na asilimia 8.51 kwa dizeli katika Bandari ya Dar es Salaam.

Pia, kuongezeka kwa gharama za uagizaji wa mafuta kwa wastani wa asilimia 7.07 kwa petroli na asilimia 25.24 kwa dizeli katika Bandari ya Tanga na zimepungua kwa wastani wa asilimia 12.64 kwa mafuta ya petroli na 12.61 kwa mafuta ya dizeli katika Bandari ya Mtwara.

Bei za mafuta za rejareja kwa maeneo mbalimbali ya miji,wilaya na mikoa ni kama zinavyoonekana hapa chini;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news