Fungeni mjadala, Rais Dkt.Mwinyi ni muumini wa kufuata Katiba na sheria za nchi

NA GODFREY NNKO

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi ni muumini wa kufuata Katiba na sheria za nchi.
Pia, imesema maoni yanayopendekeza aongezewe muda wa kubakia madarakani kwa miaka saba, badala ya miaka mitano iliyoainishwa katika Katiba ya Zanzibar sio ya Rais Dkt.Mwinyi wala sio ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Juni 24,2024 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu ya Zanzibar, Charles Hilary.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo,“Hivi karibuni kumetolewa maoni yanayopendekaza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi aongezewe muda wa kubakia madarakani kwa miaka saba badala ya miaka mitano iliyoainishwa katika Katiba ya Zanzibar.

“Maoni hayo yamekwenda mbali zaidi hata kutaka Uchaguzi Mkuu wa mwakani kumchagua Rais wa Zanzibar usifanyike, jambo hili halina tija wala faida kwa nchi yetu na Chama Cha Mapinduzi (CCM) chenye kufuata misingi ya demokrasia.

"Rais Dkt. Mwinyi ataendelea kuheshimu utaratibu uliowekwa wa Rais kuchaguliwa kila baada ya miaka mitano na amewasihi wale wote wenye mawazo tofauti na hayo wafunge mjadala huo.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news