Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo Juni 1,2024

KATAVI-Mwanafunzi mmoja wa shule ya sekondari St. Mary’s iliyopo Manispaa ya Mpanda Luis Emmanuel (17) amefariki baada ya kunywa kemikali inayodhaniwa kuwa ni ethanol katika maabara ya shule hiyo akiwa na wanafunzi wengine wawili.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi,SACP Kaster Ngonyani amesema tukio hilo limetokea mnamo Mei 25, 2024 majira ya saa 5 asubuhi ambapo amewataja wanafunzi wengine ni Evangelist Deodatus (20) na Anastazia Zakayo (17) wote kidato cha nne.

Amesema,wanafunzi hao watatu walikuwa wakifanya usafi katika maabara ya kujifunzia masomo ya sayansi kwa vitendo iliyopo shuleni hapo huku wakisimamiwa na mwalimu John Mtafya ambaye baadae alitoka nje kuendelea na shughuli nyingine za kimasomo na kuwaacha wanafunzi hao wakiendelea na usafi, ndipo walipoingia katika chumba cha kuhifadhia kemikali ambapo walichukua kemikali hiyo ya ethanol na kisha kuinywa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news