DAR-Balozi wa zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika nchi za Canada na Jamhuri ya Watu wa China na Mhariri maarufu wa vyombo vya habari nchini, Ferdinand Kamuntu Ruhinda amefariki dunia usiku wa kuamkia Juni 15,2024.
Ruhinda ambaye aliwahi kuwa Mhariri Mtendaji wa magazeti ya CCM ya Uhuru na Mzalendo, na yale ya Serikali ya Daily News/Sunday News na Habari Leo kwa nyakati tofauti, atazikwa Juni 17, 2024 kwenye makaburi ya Kondo yaliyopo Kunduchi jijini Dar es Salaam.
Ruhinda alikuwa mwanzilishi wa magazeti ya Mwananchi na Redio Uhuru na amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu akikakabiliwa na maradhi ya kisukari.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo