DAR-Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limewataka vijana wote waliohitimu Kidato cha Sita 2024 waliotakiwa kuripoti makambini kwa ajili ya mafunzo ya lazima kwa mujibu wa sheria kuanzia Juni Mosi hadi 7, 2024 na bado hawajaripoti hadi sasa, basi wafanye juu chini wakaripoti kwenye makambi waliyopangiwa mara moja wakiwa na vifaa vilivyoainishwa na jeshi hilo.
Brigedia Jenerali Hassan Mabena ambaye ni Mkuu wa Tawi la Utawala JKT ameyasema hayo Juni 22,2024 wakati akitoa taarifa ya nyongeza ya awamu ya pili ya vijana waliohitimu Kidato cha Sita kwa mwaka 2024 kujiunga na mafunzo ya lazima ambao wanatakiwa kuripoti kwenye makambi yaliyo karibu kuanzia Juni 22 hadi Juni 26, 2024.“Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele amewataka vijana waliohitimu Kidato cha Sita mwaka 2024 kuungana na vijana wenzao ili kujengewa uzalendo,umoja wa kitaifa, stadi za kazi,stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa lao.”
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo