DAR-Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeanza zoezi la kuwaondoa wadaiwa sugu walioshindwa kutekeleza matakwa ya mkataba wa ununuzi wa nyumba katika miradi yake ya Dar es Salaam. Zoezi la kuwaondoa wadaiwa sugu hao lilifanyika tarehe 18 Juni 2024 katika mradi wa nyumba za Kijichi, Temeke.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Meneja Miliki wa NSSF, Geofrey Timoth amesema zoezi la kuwaondoa wadaiwa sugu walioshindwa kulipa madeni yao ya muda mrefu katika nyumba za NSSF ni endelevu katika miradi yote.
Timoth amesema kuwa NSSF ilitoa notisi ya siku 30 na baadaye ilitoa siku 14 ya kuwataka wadaiwa hao kulipa madeni yao lakini hawakulipa, hivyo baada ya kujiridhisha na kufanya tathimini, NSSF ilifanya maamuzi ya kuwatoa wadaiwa sugu katika nyumba zake ili kutoa fursa kwa wananchi wengine kununua nyumba hizo kwa utaratibu wa mpangaji mnunuzi.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo