IRINGA-Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imepongezwa kwa kuendeleza jitihada mbalimbali za kuboresha miundombinu katika Sekta ya Utalii nchini ambapo kwa sasa kupitia Mradi wa REGROW inatekeleza ujenzi wa Kituo cha Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) Kihesa Kilolo mkoani Iringa kitakachosaidia hifadhi za Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini.
Mhandisi Mshauri na Meneja wa mradi huo wa ujenzi wa kituo hicho cha TAWIRI,Wilfred Saitoria amebainisha kuwa juhudi anazozifanya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan zinapaswa kuendelezwa na wao kama watekelezaji wanamuunga mkono Mhe. Rais kwa kuhakikisha wanatekeleza ujenzi huo kwa weledi ambapo mradi huo mpaka kukamilika kwake utagharimu zaidi ya shilingi bilioni moja.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo