Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo Juni 26,2024

PWANI-Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, Mheshimiwa Petro Magoti amepiga marufuku watu kuandaa shughuli za ngoma kama vile mdundiko, unyago na sherehe za muziki na kuruhusu wanafunzi kujumuika na kuserebuka kwenye shughuli hizo.

Mheshimiwa Magoti amemuagiza Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kisarawe kwamba vitendo hivyo vikibainika akamate kuanzia mpiga ngoma,wazazi wa mtoto, aliyepewa tenda ya muziki hadi gari lililobeba muziki huo ili liende wilayani.

Magoti ameyasema hayo wilayani Kisarawe wakati akikabidhiwa ofisi rasmi na DC Fatma Nyangasa huku akiwataka walimu wanaoanzisha mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi wao kujiandaa, kwani akiwabaini atawashughulikia.
“Kama mtu anapewa tenda ya kuchezesha ngoma kwa wanafunzi waambie wasiende, tutakamata gari, tunafika Polisi pale usiku tunatoboa matairi upepo hamna muziki utaletwa hapa halmashauri, sasa utatuambia DC kapokonya vitu si kuna sheria ya kuhatarisha, sikiliza ile clip ya Mheshimiwa Mkuchika ameelezea vizuri mtu anayehatarisha amani kwa sababu wewe unafanya watu wawe wajinga wasisome unahatarisha amani, tunadili na wewe vizuri sana.

“Nimesikia kuna walimu wanapenda wanafunzi, sitaki kuwahukumu sijafika, naendelea kupokea data zangu kama wewe unatafuna watoto wetu ambao yaani wewe, Mheshimiwa Rais analeta pesa yule mtoto anakula anavaa anapendeza, yaani Mheshimiwa Rais anatoa matumizi wewe unakula, serious? Halafu Mheshimiwa Rais anakulipa mshahara, umepewa nyumba ya Serikali unaishi, umeme upo.
“Mtu wa Maendeleo ya Jamii upo wapi? Malezi hapa ni zero,una watoto? Mwanao yupo darasa la ngapi? Chekechea?. Sasa fikiria mwanao yupo darasa la tatu akapigwa mimba utajisikiaje? Si vibaya? ndio Rais anavyojisikia vibaya hivyo, kusikia watoto wana mimba, kwa hiyo andaa utaratibu wa semina na mikutano ya darasa la maadili kuanzia Julai, mwaka huu kila shule tuwe na mambo ya maadili.

"Mtu yoyote anayetaka kuweka nguvu kuhusu unyanyasaji wa kijinsia twende nae, ukiona Mtu ananyemelea kabinti kashule njoo niambie huyu alikuwa na mtoto nimemuona anamshika chuchu tutamshughulikia vibaya mno,” amesema DC Magoti.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news