DODOMA-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa amesema Ofisi ya Rais-TAMISEMI haitasita kuchukua hatua kwa kiongozi yeyote anayewanyanyasa wananchi kupitia ukusanyaji wa ushuru wa mazao, kwani Serikali imeshatoa miongozo kuhusu ukusanyaji wa ushuru wa mazao.
Mheshimiwa Mchengerwa ameyasema hayo Juni 26,2024 wakati akichangia hoja yake bungeni jijini Dodoma katika Bunge la Bajeti ya mwaka 2024/2025 linaloendelea.
“Yapo maeneo ambapo tunaona kuna hitilafu katika ukusanyaji wa ushuru wa mazao, tutafika huko katika halmashauri zenye changamoto hizo, maelekezo yangu watanzania wasiyanyasike kwenye maeneo yao na TAMISEMI hatutasita kuchukua hatua kwa kiongozi yeyote anayewanyanyasa Watanzania katika maeneo yetu,kwani Serikali ilikwisha kutoa muongozo.”
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo