GEITA-Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imefanikiwa kufikia halmashauri zaidi ya 60 nchini katika utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP). Utekelezaji wa mradi huo unahusisha utambuzi wa kila kipande cha ardhi, upangaji wa maeneo yote yaliyotambuliwa kwa kuandaa michoro ya mipango miji, upimaji wa viwanja vilivyopangwa kwa kuweka alama za upimaji na kuandaa ramani za upimaji na wananchi kumilikishwa maeneo yao kwa kupewa hatimilki.


Hayo yamebainishwa Juni 27,2024 na Mkuu wa Wilaya ya Bukombe,Mhe. Paskasi Muragili wakati wa ufunguzi wa kikao cha kujadili utekelezaji wa mradi wa LTIP katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo