ARUSHA-Juni 3, 2024 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Amosi Makalla amemshauri aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Nyasa ambaye pia ni Mbunge wa zamani wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa ahamie CCM kufuatia sakata linaloendelea baada ya Msigwa kulalamikia kutotendewa haki kwenye uchaguzi wa uenyekiti wa CHADEMA Nyasa uliompa ushindi,Joseph Mbilinyi (Sugu).
"Msigwa amesema...najitokeza hadharani kuwaeleza Watanzania na CHADEMA sisi muda wote tumehoji Tume ya Uchaguzi kumbe sisi ni waongo, hata sisi wenyewe hatufuati taratibu za uchaguzi. Mimi nimeonewa nimeibiwa kura...sasa na mimi namuambia Msigwa pole sana Mchungaji njoo CCM ambako kuna demokrasia tele, kuna uwazi.
“Umeonewa pole sana Mchungaji Msigwa hicho chama hakikufai tena njoo CCM, amesema tunawadanganya tu watu kuhusu Katiba, Tume ya Uchaguzi kumbe chama chetu hakifuati hata sheria za uchaguzi za Chama chake.”
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo