DAR-Innocent Chengula (23) mkazi wa Kigogo Luhanga jijini Dar es Salaam amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam baada ya kutiwa hatiani kwa makosa sita ikiwemo kujipatia kwa njia ya udanganyifu shilingi milioni nne kutoka kwa Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete ambaye ni Mbunge wa Chalinze na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti na Utumishi wa Umma na Utawala Bora.Uamuzi huo umetolewa Juni 5,2024 na Hakimu Mkazi Mkuu, Yusto Ruboroga na kuamuru pia mshtakiwa huyo arudishe shilingi milioni nne za Naibu Waziri huyo.
Ilidaiwa Julai 26, 2022 mshtakiwa alijitambulisha kuwa yeye ni Katibu Mkuu Dkt.Hassan Abbas na kwamba mama yake ni mgonjwa sana, hivyo anahitaji msaada wa fedha kwa ajili ya kugharamia matibabu yake ambapo kwa uungwana wake bila kusita, Naibu Waziri Ridhiwani Kikwete alimtumia pesa hiyo shilingi milioni nne.
Mbali na adhabu hiyo, pia Mahakama ya Kisutu imeitaifisha simu moja ya mkononi pamoja na laini tatu za simu alizokuwa akitumia mshtakiwa huyo na kuwa mali ya Serikali ambapo.
Chengula ambaye ni Mkazi wa Kigogo Luhanga jijini Dar es salaam, alikuwa anakabiliwa na mashtaka sita yakiwemo ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutuma ujumbe wa maandishi kwenda katika mtandao wa kijamii wa WhatsApp ambapo alijitambulisha kwa Ridhiwani Kikwete na Rais wa TFF Wallace Karia kuwa yeye ni Dkt. Hassan Abbas (Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii).
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo