Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo Juni 30,2024

IRINGA-Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa limesema,ajali iliyohusisha pikipiki na gari aina ya Faw mali ya Kampuni ya TRANSAFRICA imesababisha vifo vya watu wanne akiwemo dereva wa pikipiki hiyo na abiria watatu,miongoni mwao ni mtoto mwenye umri wa miaka mitano ambao wote ni wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Ipogolo mkoani humo.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, ACP Alfred A. Mbena amesema, "Juni 28,2024 usiku eneo la Mlima Ipogolo, Kata ya Kitanzini, mkoani Iringa katika barabara Kuu ya Iringa - Dodoma, pikipiki ambayo ilitoroshwa mara baada ya ajali kutokea ikiendeshwa na Hassan Buruhani (17) mkazi wa lpogoro akiwa amebeba abiria watatu, Helena Thomas (12) wanafunzi wa darasa la saba,

"Ally Tenywa (09) Mwanafunzi wa darasa la kwanza na Gabriel Gongo (05) mwanafunzi wa awali wote kutoka Shule ya msingi Ipogolo iligonga ubavuni upande wa kushoto wa gari namba RAG450N/RL 5167 aina ya FAW mali ya kampuni ya TRANSAFRICA ikitokea mkoani Ruvuma kuelekea Dodoma ikiendeshwa na Said Rashid (27) mkazi wa Dar es salaam na kusababisha vifo kwa dereva wa pikipiki na abiria wote watatu.”

Amesema,kutokana na chunguzi,wamebaini kuwa, chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa Dereva wa pikipiki kujaribu kulipita gari hilo upande wa kushoto na kugonga ubavuni, kuanguka na kisha kukanyagwa na gurudumu za nyuma za gari hilo
.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news