ARUSHA-Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Paul Makonda amemuagiza Mkuu wa Polisi wa Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kutokamata magari ya utalii kwenye mkoa huo na badala yake ukaguzi kwa watalii ufanyike kwenye mipaka na kwenye viwanja vya ndege vinavyotumika na watalii ili kuepusha usumbufu.
Ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari Juni 8, 2024 kwenye Viwanja vya Magereza Kisongo kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya Karibu Kili Fair 2024, yanayojumuisha makampuni zaidi ya 700 ya kimataifa kutoka kwenye mataifa zaidi ya 50. "Kama Serikali ya Mkoa tumeona tuweke mazingira bora zaidi ya kuhakikisha kwamba mtalii anapokuja kwenye mkoa wetu hapati changamoto na ajisikie kuheshimika kwa sababu Taifa limejiandaa kupokea watalii, kuanzia tarehe moja mwezi wa saba tumekubaliana kwamba hakuna polisi kusimamisha gari la utalii.”
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo