DAR-Rais wa Young Africans Sports Club (Yanga),Mhandisi Hersi Said amewahakikishia wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kwamba, msimu unaokuja utakuwa bora kwa klabu na benchi litakuwa imara kuliko msimu uliopita huku wachezaji wakiongezewa nguvu.
Ameyasema hayo Juni 9,2024 katika Mkutano Mkuu wa Yanga uliofanyika jijini Dar es Salaam ambapo msimu ujao wanatarajia kutumia zaidi ya shilingi bilioni 20.




“Tulifanikiwa kutinga hatua ya robo fainali na kutolewa kwa matuta na Bingwa wa AFL na kigogo wa soka Afrika Kusini, Mamelodi Sundown, hata hivyo katika mchezo tulifunga bao halali ambalo Rais wa Soka Afrika, Dkt. Patrice Motsepe amenukuliwa akisema kuwa lilikuwa goli halali."
Tags
Habari
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo