HakiElimu yazindua ripoti ya utafiti kuhusu hali ya upatikanaji wa elimu

DAR-Asasi ya Kiraia nchini iitwayo HakiElimu imezindua Ripoti ya Utafiti kuhusu hali ya upatikanaji wa elimu bora kwa watoto wanaoishi katika Makazi duni na yasiyo rasmi, Mijini ambao unatarajia kusaidia kuboresha upatikanaji wa elimu kwa watoto wanaoishi katika makazi duni nchini Tanzania.
Utafiti huo wa HakiElimu umefanywa kwa kushirikiana na Kituo cha Utafiti wa Idadi ya Watu na Afya Afrika ‘APHRC’, chenye makao yake makuu jijini Nairobi ambapo utafiti huo umefanyika mwaka 2022 katika mazingira duni ya mijini na umeifikia mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma.

Akizungumza wakati akizindua ripoti hiyo kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, Mkurugenzi Uthibiti Ubora, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Ephraim Simbeye amesema mpango wa Maendeleo ya Sekta Elimu wa Miaka Mitano 2021/22-2025/26 unagusia Elimu ya mjini.
Ndugu Simbeye ametoa wito kwa HakiElimu na wadau wengine kuendelea kufanya tafiti na kuziwasilisha kwa umma kwani unatoa nafasi kwa wadau mbalimbali pamoja na Serikali kutumia matokeo yake katika kufanya maamuzi ambayo yanajengwa katika Ushahidi wa Kisayansi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa @HakiElimu Dkt John Kalage amesema HakiElimu ilisukumwa kufanya utafiti huo kwa lengo la kupata hali halisi ya upatikanaji wa elimu katika maeneo ya mijini na kuikuza dhana ya elimu ya mjini “Urban Education” kama eneo la kitaaluma na utafiti.
Naye Mwakilishi wa Kituo cha Utafiti wa Idadi ya Watu na Afya Afrika ‘APHRC’ Ndugu Francis Kiroro ametaja sababu za uchaguzi wa maeneo yaliyofanyika utafiti huo “Inakadiriwa kuwa ifikapo mwaka 2050, asilimia 55 ya watu Tanzania watakuwa mijini, huku Dar Es Salaam ikiongoza kwa ongezeko la watu mijini baraka Afrika, hivyo mipango madhubuti inahitajika”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news