Mkusanya mapato hatiani kwa kupuuza wajibu wa kikazi

KAGERA-Mahakama ya Wilaya Karagwe mkoani Kagera imemtia hatiani Afisa Mifugo wa Kijiji cha Nyaishozi, Mwenge Datius Mathias kwa kupuuza wajibu wa kikazi.
Mshtakiwa ametiwa hatiani kwa kosa la kupuuza wajibu wa kikazi kinyume na kifungu cha 123 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu.

Aidha,amepewa adhabu ya kutofanya kosa ndani ya miezi 12 (conditional discharge) na kurejesha fedha za halmashauri shilingi 2,282,500.

Fedha hizo hakuwa ameziweka benki baada ya kukusanya kwa njia ya POS ambapo ameamriwa ndani ya miaka mitatu awe amekwishazilipa.

Hukumu hiyo katika shauri la jinai Namba 14808/2024 imetolewa Juni 20,2024 na Mheshimiwa Flora Haule, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Karagwe.

Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili Mwandamizi Richard Malekano huku mshtakiwa akijiwakilisha mwenyewe.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news