Hawa hapa watumishi 10 waliofikishwa Mahakamani kwa tuhuma za upigaji Mwanza

MWANZA-Watumishi 10 wa nafasi na kada mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Sengerama mkoani Mwanza wamefikishwa mahakamani kwa makosa ya matumizi mabaya ya madaraka,ufujaji na ubadhirifu wa shilingi millioni 87.
Kwa pamoja wanatuhumiwa kutenda makosa hayo kinyume na vifungu vya 31 na 28 vya PCCA sura ya 329 na marejeo yake ya mwaka 2022.

Mashauri 10 dhidi ya watumishi hao wa Serikali yamefunguliwa Juni 3,2024 mbele ya Hakimu Mwandamizi Mfawidhi, Mheshimiwa Evod Eugen Kisoka.

Aidha, yamesomwa mahakamani hapo na Waendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Wakili Moses Malewo, Saida Salum na Maxmillian Kyabona.

Washtakiwa hao kwa nyakati tofauti kati ya Julai Mosi, 2016 hadi Februari 15,2021 wanadaiwa wametenda makosa hayo wakiwa na nia ovu.

Imedaiwa walitumia madaraka yao vibaya na kushindwa kuwasilisha fedha za mapato ya Serikali zaidi ya shilingi millioni 87 kwenye akaunti ya Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.

Mapato hayo ni makusanyo mbalimbali fedha za Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema.

Kitendo cha kutokuwasilisha Benki fedha hiyo ya Serikali ni kinyume na kifungu cha 50(5) ya Memoranda ya Fedha za Halmashauri za Mwaka 2009, ambazo kimsingi walijipatia manufaa binafsi.

Baadhi ya watumishi waliofikishwa Mahakamani ni;

1. Revocatus Reuben Kasana mwenye shauri namba 14931/2024

2. Francisca Mathew Temu mwenye case namba 14927/2024

3. Elias Amos Magulu mwenye case namba 14942/2024

4. Kalambizi Leonard Gervase mwenye case namba 14924/2024

5. Benedict Kanfune Phillip mwenye case namba 14922/2024

6. Faida Revocatus Majaliwa mwenye case namba 14932/2024

7. Emmanuel Magida Mwitagula mwenye case namba 14920/2024

8. Felix Chacha Boniphace mwenye case namba 14921/2024

9. Jenipher Maige Mashamba mwenye case namba 1433/2024 na

10. lluminata Samwel Suleiman mwenye case namba 14930/2024.

Washtakiwa wote wamekana makosa yao na wapo nje kwa dhamana.

Kesi hizo zitatajwa tena mahakamani Juni 19 na 26, 2024 kwa ajili ya hoja za awali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news