Huyu hapa Richard Hindorf

NA MWANDISHI WETu

WAKATI wa vita ya kwanza ya dunia, mwaka 1915, aliingia vitani kwenye jeshi lililokuwa chini ya kamanda Paul von Lettow-Vorbeck, alishiriki katika upinzani maarufu wa askari wa kijerumani katika ukoloni huo mpaka mwisho. 

Hata hivyo, alishikwa na Serikali ya Uingereza pale Dar es salaam mwaka 1917 na kisha kuswekwa lupango.
Alikuwa mwanasayansi Mjerumani mtaalmu wa kilimo na msafiri. Alishughulika sana katika kufanya kazi pembezoni mwa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani katika maisha yake.

Kwa hamu ya kuona nchi za wakoloni alitembelea,Java, Sumatra, Australia, Ceylon na Misri, alifika Afrika Mashariki ya Ujerumani mwaka 1891, na baadaye, alirudi nchini mara kwa mara katika maisha yake.

Awali, alianzisha shamba la kahawa kule Derema, kwenye milima ya Usambara, alitoka na kwenda safari ya Afrika ya Magharibi, Afrika Kusini, Msumbiji na Kameruni.

Richard Hindorf alizaliwa nchini Ujerumani, Novemba 17 mwaka 1863 na kufariki huko Berlin, Dahlem, Mei 13 mwaka 1954. Baba yake, Heinrich, alikuwa mwalimu wa shule. Baada ya kumaliza shule, alifika Chuo cha Halle kusoma masomo ya kilimo na sayansi ya siasa.

Akafanya kazi huko New Guinea, ambako alisimamia kituo kikuu cha mashamba ya Kampuni ya New Guinea, toka mwaka 1887 hadi mwaka 1889.

Mchango wake muhimu wa kilimo akiwa Afrika Mashariki ulikuwa ni kuanzisha kilimo cha mkonge, hasa katika eneo la Usambara Mkoa wa Tanga. Mwaka 1892 mpaka mwaka 1893, alisoma kule Bulletin ya Kew namba 62, kuhusiana na mmea wa mkonge aina ya Agave sisalana, ambao hupatikana nchini Mexico.

Mmea huu uliweza kustawi katika mazingira ya hali ya hewa ya Tanganyika sawa na Mexico, na alijaribu kupanda mkonge wa kwanza ulioletwa kutoka Florida, karibu na mdomo wa Mto Pangani.

Mafanikio yasiyokuwa na tumaini ya mashamba ya mkonge mwishowe yalisababisha bidhaa hiyo kuwa zao kuu la nchi na kisha Tanganyika kuliuza nje kwa miaka mingi na kuwa chanzo kikubwa cha mapato kwa uchumi wa nchi, hatimaye Tanganyika ikawa muuzaji mkubwa wa zao la mkonge kuliko nchi yoyote nyingine duniani.

Mchango wake mwingine muhimu ulikuwa katika uanzishwaji wa Taasisi ya Utafiti ya Amani. Mwaka 1890, katika gazeti la Kijerumani, alileta wazo la kuanzisha kituo cha utafiti katika koloni la Afrika Mashariki ya Kijerumani kama vile vituo vingine vilivyoanzishwa katika makoloni ya Uingereza na Uholanzi.

Hindorf mwenyewe alikuwa mshiriki mwenza wa Kamati ya Uchumi ya Kikoloni, mwaka 1898 kamati hiyo ilikusanya fedha huko Berlin kwa lengo la kuanzisha na kuendesha kituo hicho cha utafiti cha kanda ya kitropiki katika milima ya Usambara.

Kwa msaada wa mwanabotania Mjerumani, Franz Stuhlmann, kituo hicho kilijengwa huko Amani, Wilaya ya Muheza, katika milima iliyoko Magharibi mwa Usambara, pamoja na bustani kubwa yenye mimea na miti.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news