INEC yakabidhi vyama vya siasa orodha ya vituo vya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura

DAR-Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imevikabidhi vyama vya siasa orodha ya vituo vya uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga Kura nchini.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji (Rufaa), Jacobs Mwambegele akikabidhi nakala ya orodha ya vituo vyote vya kuandikisha wapiga kura kwa viongozi na wawakilishi wa Vyama 19 vyenye usajili kamili wakati Vyama hivyo vilipokutana katika mkutano wa Tume na viongozi wa vyama vya siasa uliofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 07 Juni, 2024 ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uboreshaji wa Daftari.

Mapema wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo, Jaji Mwambegele aliahidi kuvipatia nakala hiyo vyama vyote na pia Vyama hivyo vitapatiwa nakala tepe ya orodha hiyo.


“Leo kila chama kitapewa nakala ya orodha ya vituo vyote vya kuandikisha wapiga kura. Dhumuni la kuwapatia nakala hizo ni kuwawezesha kupanga na kuweka mawakala wa uandikishaji katika vituo vya kuandikisha wapiga kura,”amesema Jaji Mwambegele.

Vyama hivyo vilivyopokea ni AAFP, ACT - WAZALENDO, ADA - TADEA, ADC, CCK, CCM, CHADEMA, CHAUMA, CUF, Demokrasia Makaini, DP, NCCRA- MAGEUZI, NLD, NRA, SAU, TLP, UDP, UMD na UPDP.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news