INEC yatoa vibali kwa asasi 191 elimu ya mpiga kura na uangalizi

NA GODFREY NNKO

TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetoa vibali vya kutoa elimu ya mpiga kura na uangalizi wakati wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa asasi 191 nchini.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Juni 25,2024 na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa INEC,Ramadhani Kailima.

"Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi katika kikao chake cha tarehe 22 na 24 Juni 2024,kwa kuzingatia Kifungu cha 10 (1) (g) na (h) cha Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Na.2 ya mwaka 2024.

"Ikisomwa pamoja na Kanuni ya 46 (4) ya Kanuni za uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga za mwaka 2024 imetoa vibali vya kutoa elimu ya mpiga kura wakati wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa asasi za kiraia 157.

"Na kibali cha uangalizi wakati wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa asasi 34 za ndani ya nchi."

Kailima ameeleza kuwa, asasi zilizopewa kibali cha elimu ya mpiga kura zitajulishwa kwa njia ya barua pepe kupitia mfumo wa usajili.

Lengo ni ili ziweze kujaza taarifa za kuweza kukamilisha taratibu nyingine ikiwemo kutaja maeneo ambayo watatoa elimu hiyo na orodha ya watu watakaotoa elimu ya mpiga kura katika maeneo hayo.

"Majina ya taasisi na asasi za kiraia zilizopata kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura na uangalizi wakati wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura 2024/2025 yatatangazwa kupitia tovuti ya tume (www.inec.go.tz) na mitandao ya kijamii."

Vilevile tume hiyo imewapongeza wote waliopata vibali kwa ajili ya kutoa elimu ya mpiga kura na kuwa waangalizi wa uandikishaji kwa mwaka 2024/2025.

Kumbuka kuwa, maboresho ya Daftari la Kudumu la Wapiga Kura nchini yataanza mwezi Julai, mwaka huu huku kaulimbiu ikiwa ni Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura Ni Msingi Wa Uchaguzi Bora.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news