Jamii yatakiwa kuwapeleka watoto shule

NA RESPICE SWETU

JAMII wilayani Kasulu mkoani Kigoma imetakiwa kuwapeleka watoto wote shuleni bila kuwabagua walio na mahitaji maalumu.Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasulu, Paul John wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika kiwilaya katika Kijiji cha Makere wilayani Kasulu.

Akisoma hotuba ya maadhimisho hayo amesema, chimbuko la kufanyika kwa siku ya mtoto wa Afrika ni kutokana na mauaji ya kikatili ya watoto wapatao elfu mbili yaliyotokea katika Kitongoji cha Soweto nchini Afrika Kusini.
Amesema, watoto hao waliokuwa katika maandamano ya kudai haki ya kupatiwa elimu iliyo bora na inayofanana na mila na desturi za Kiafrika, waliuwawa kikatili na serikali ya kikoloni na ya kibaguzi iliyokuwa ikilitawala taifa hilo.

“Katika kuonesha kuwa ukatili huo haukubaliki, serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dr. Samia Suluhu Hassani, imeboresha miundo mbinu ya kielimu kuwawezesha watoto wote wenye umri wa kwenda shule wanapatiwa haki hiyo.

"Elimu jumuishi kwa watoto izingatie maarifa, maadili na stadi za kazi,tumekusudiwa kutoa chachu kwa wazazi na jamii kuhakikisha kila mtoto anapelekwa shule bila kuwepo ubaguzi wa aina yoyote.
Maadhimisho hayo ya kiwilaya yaliyofadhiliwa na shirika la World Vision Tanzania, yaliambatana na mdaharo uliowahusisha watoto na wadau kutoka katika maeneo mbalimbali.

Miongoni mwa mada zilizowasilishwa wakati wa mdahalo huo ni pamoja na dhima ya maadhimisho ya mtoto wa Afrika, elimu ya ulinzi wa mtoto, mimba za utotoni, lishe kwa watoto na ushiriki wa jamii katika mapambano ya kupinga ukatili wanaofanyiwa watoto.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news