NA HUPHREY SHAYO
Msakuzi Kaskazini
TUNAISHi katika wilaya ambayo mkuu wa wilaya kipaumbele chake ni kuingia nyumba za kulala wageni kupambana na madada poa na kwenye madamguro.
Wakati wilaya hii asilimia 80 ya barabara zake za mtaa ni mbovu,asilimia 70 ya mitaa tunayoishi ina shida ya maji na uchafuzi wa nazingira.
Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan amewateua vijana kuja kutatua kero za wananchi zinazogusa maisha yao ya kila siku, lakini cha ajabu viongozi hawa wamekuwa watu wa kick na kuacha kumsaidia Mheshimiwa Rais.
Tangu DC wetu Hassan Bomboko aletwe kwenye wilaya yetu, yeye amekuwa mtu wa kusafiri na hata aliporejea ameshindwa kuja kutatua matatizo yetu wananchi kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake Hashim Komba ambaye alimudu vyema wilaya hii.
Licha ya matatizo ya kukwama kwa miradi ya maji na barabara kuwa mbovu mitaani kwetu, tumeshangaa kila siku tukiona DC huyu kupambana na madanguro wakati bado Ubungo ina mahitaji ya msingi sana.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) anasema, Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ilitoa kiasi cha shilingi 218,800,000 kwa vikundi 23.
CAG alipokwenda kukagua vikundi 23 vilivyotajwa na kutaka kuona miradi yao, alikuta wamegawana shilingi 218.8 milioni. HAKUNA MRADI HATA MMOJA.
CAG aligundua kuna watu wamefanya kazi hawajalipwa pesa zao TZS 7.8 bilioni. Kituko Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo pekee haijalipa TZS 6.7bn.
Baraza la Madiwani Manispaa Ubungo na Waziri wa TAMISEMI walidanganywa na DED amekusanya Mapato ya TZS 27, 868,406,661.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alipokwenda Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kukagua akakuta ilikusanywa TZS 24,414,268,232.
Tofauti ya TZS 3,454,148,429. Hizi ni BILIONI TATU. Mkuu wa Wilaya anatakiwa kupambana na UFISADI kama huu, siyo kupambana na madada poa hao.
Tujiulize, watu wa halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, wanakereka na hao machangudoa kwa kiwango gani? Tatizo lao siyo huduma za jamii ni machangudoa?.
Kama kuna binadamu anaona huyu DC anachapa kazi kwa kucheza na madada poa basi tupo katika mikono ya wahuni na wananchi wake ni mazombi kabisa.
Mwandishi wa habari hii ni mkazi wa Manispaa ya Ubungo, ni miongoni mwa wakazi ambao wanafahamu historia ya Manispaa hii vema.