Katibu Tawala,Tixon Tuyangine Nzunda afariki katika ajali Kilimanjaro

KILIMANJARO-Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro,Tixon Tuyangine Nzunda, amefariki dunia katika ajali iliyotokea barabara Kuu ya Moshi kwenda Arusha.
Ajali hiyo imetokea leo mchana Juni 18, 2024 wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mheshimiwa Nurdin Babu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo pia imemuua dereva wake.

Machi 2023, Nzunda aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro akichukua nafasi ya Willy Machumu ambaye alistaafu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news