DAR-Kwa kutambua umuhimu na changamoto wanazopitia watoto kote duniani, Afrika pamoja na Tanzania, hasa za kunyanyaswa kingono, kutumikishwa, kupigwa na kuuwawa, kusafirishwa, kubaguliwa na kutengwa hasa watoto wenye mahitaji maalum, Chuo cha Ustawi wa Jamii nchini kimeanzisha kozi ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto.
Ni kozi ambayo inatolewa kwa ngazi ya cheti mpaka stashahada kwa lengo la kutatua changamoto za watoto wa kitanzania za ukosefu wa wataalam wenye ujuzi wa kuwasaidia watoto wanapokuwa au wanapopatwa na shida katika vituo vya kulelea watoto mchana.
Vilevile, hospitali, masokoni, mitaani na sehemu nyingine katika jamii yetu ila kuhakiisha mtoto anakuwa katika utimilifu wake( kimwili, kiakili, kijamii na kimaono).
Aidha,Chuo cha Ustawi wa Jamii kitaendelea kuwa mdau katika kuhakikisha ustawi wa mtoto wa Kitanzania na Kiafrika.