Maendeleo ya sayansi na teknolojia yaendelee kuleta matokeo chanya-Waziri Mhagama

DAR-Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mheshimiwa Jenista Mhagama ameomba wanawake kuendelea kuliombea Taifa na kuombea kizazi kilichopo na kizazi kijacho ili kiendelee kuwa na hofu ya Mungu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akishiriki katika maombezi maalumu yaliyoongozwa na Mhashamu Askofu Dkt. Barnabas Mtokambali (kulia) na Mhashamu Flora kaguo na Wahashamu Maskofu wengine kwenye Kongamano la Wanawake la (CPCT) Taifa lilofanyika Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Ametoa kauli hiyo Mei 31,2024 wakati akihutubia Kongamano la Wanawake wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania ambalo limefanyika Sasaba jijini Dar es Salaam likiongozwa na kauli mbiu yake inayosema, Mwanamke ni Jeshi kubwa kwa Kanisa na Taifa.
Ameeleza kwamba,mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia yanapaswa kuendelea kutusaidia kumjua Mungu kwa haraka na hayapaswi kutuingiza kwenye changamoto za kidunia.
"Licha ya kwamba nchi yetu haiegemei upande wowote katika masuala ya dini (Secular State), lakini sehemu kubwa ya watu wake wanaamini katika Mungu kupitia dini na madhehebu mbalimbali.

“Tukifanya kazi hii vizuri tutakuwa tumelitendea haki Taifa, na naomba niendelee kutoa wito kwa wakinamama na watoto (CPCT) muendelee kubaki imara kwenye kanisa na Taifa letu,” alihimiza Waziri Mhagama.
Waziri Mhagama amezungumzia pia uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambapo ametoa rai kwa wakinamama kuombea uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu, ili chaguzi hizo zipite salama na washawishi wanawake wenye uwezo wagombee.

“Mwanamke akipata nafasi ya kuongoza kijiji au mtaa na akiwa ametoka kwenye jeshi kubwa la kuliombea Taifa atafanya kazi kwa weledi,” alibainisha.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT), Mhashamu Askofu,Dkt.Barnabas Mtokambali amesema umoja huo uliundwa na Hayati Ali Hassani Mwinyi aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili ambaye aliridhia kuundwa kwa Umoja wa Baraza hilo mwaka 1993 na makao yake makuu yalikuwa jijini Dar es Salaam.

“Baraza hili lina baraka zote za madhebu ya Kipentekoste na baraka za nchi na tumeunda Idara na Mabaraza kwenye ngazi za mikoa na wilaya ikiwemo idara hii ya wanawake ambayo inatimiza maono, na dhima iliyokusudiwa," alisema Mhashamu Askofu Dkt. Barnabas Mtokambali.
Ikumbukwe Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT) limetimiza miaka 31 tangu kuundwa kwake, na lina idara tisa ikiwemo Idara ya Wanawake wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania lenye maono ya kuwa na wanawake wa Kipentekoste wanaotembea katika nguvu ya Roho Mtakatifu na kuubadilisha ulimwengu kwa Injili ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo, na hili ni Kongamano la kwanza la Wanawake wa CPCT Taifa kufanyika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news