DODOMA-Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Kheri Mahimbali ameiagiza Tume ya Madini chini ya Katibu Mtendaji wake, Mhandisi Yahya Samamba kuongeza kasi ya kutatua migogoro ya wachimbaji wa madini nchini.
Mahimbali ametoa maelekezo hayo leo Juni 27, 2024 alipotembelea Banda la Tume ya Madini katika Maonesho ya Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA) yanayoendelea katika Viwanja vya Jakaya Convention Centre (JKCC) jijini Dodoma.

"Msi -ignore wachimbaji wadogo, STAMICO hata kama ni walezi na nyie Tume mna 'role' yenu, "amesema Mahimbali.