Makamu wa Rais agusia mambo muhimu kuliepusha Taifa dhidi ya jangwa

DODOMA-Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango amesema ili kufanikisha juhudi za kuhuisha ardhi iliyoharibiwa, kujenga ustahimilivu dhidi ya ukame na kuzuia kuenea kwa jangwa ni muhimu Taifa liimarishe menejimenti na usimamizi wa mazingira ikiwemo kupima na kuzingatia matumizi bora ya ardhi pamoja na kubadili mfumo wa ufugaji.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakati alipowasili katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Dodoma kushiriki Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani tarehe 05 Juni 2024.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete mkoani Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Mazingira na Usimamizi wa Kijamii wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Bi. Zafarani Madayi kuhusu miradi mbalimbali ya upandaji miti pembezoni mwa Barabara wakati akikagua mabanda ya maonesho katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Dodoma tarehe 05 Juni 2024.

Amesema inahitajika wafugaji kuanza kufuga kisasa kwenye mashamba yao ya mifugo na kudhibiti idadi kubwa ya mifugo inayozidi uwezo wa upatikanaji wa malisho.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) Dkt. Ladislaus Chang’a kuhusu maboresho yaliyofanywa katika taasisi hiyo yanayowezesha utabiri sahihi wakati akikagua mabanda ya maonesho katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Dodoma tarehe 05 Juni 2024.

Pia amesisitiza umuhimu wa kubadili kilimo ili kiwe endelevu na cha kisasa zaidi, kinachozingatia matumizi ya mboji na marejea, matumizi ya matandazo ya majani ili kuhifadhi unyevu, matumizi ya teknolojia za kijani pamoja na kudhibiti uchomaji hovyo wa misitu na vichaka.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akishuhudia bidhaa mbalimbali zinazozalishwa kutokana na taka za plastiki alipotembelea banda la Umoja wa Wazalishaji Vinywaji (PETPro) wakati akikagua mabanda katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Dodoma tarehe 05 Juni 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa mara baada ya kukagua mabanda ya maonesho katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Dodoma tarehe 05 Juni 2024.

Halikadhalika Makamu wa Rais ameziagaiza Halmashauri zote nchini kusimamia ipasavyo utekelezaji wa sheria ndogo za kulinda mazingira na kuhakikisha hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi ya wanaokwenda kinyume na sheria hizo.

Amewasihi viongozi wa Serikali, Bunge, Chama, Dini na Asasi za kiraia kuungana katika kupaza sauti ili kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira.

Aidha, Makamu wa Rais ametoa rai kwa Halmashauri zote kufanya jitihada kuhamasisha na kuvutia viwanda vyenye teknolojia ya kubadili taka za aina mbalimbali ili ziweze kutumika tena kama bidhaa.

Pia ametoa wito kwa wananchi na sekta binafsi kuchangamkia fursa zilizopo katika ukusanyaji na urejelezaji wa taka hapa nchini.
Makamu wa Rais amesema ili kufanikiwa kupunguza na hatimaye kukomesha kabisa uharibifu wa mazingira ni lazima kutafsiri maneno kuwa vitendo katika ulinzi ,usimamizi, na utunzaji wa mazingira na kuimarisha ushirikiano wa dhati kati ya Serikali, Asasi zisizo za Kiserikali, Sekta Binafsi,Wasanii, Taasisi za Kidini, Viongozi wa Mila na wananchi kwa ujumla.

Makamu wa Rais amesema katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira, Serikali imechukua hatua mbalimbali zinazojumuisha kupitishwa kwa Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021, Mpango Kabambe wa Taifa wa Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (2022-2032) na kuongeza kasi ya upimaji na umilikishaji wa ardhi kimila na uhamasishaji wa matumizi endelevu ya ardhi hususan kilimo mseto, kilimo cha matuta, kilimo hifadhi na mbinu endelevu za kiasili za hifadhi ya malisho,bahari, maziwa na rasilimali nyingine za maji.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Dodoma tarehe 05 Juni 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimkabidhi Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Sera ya Uchumi wa Buluu ya Mwaka 2024 mara baada ya kuizindua wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Dodoma tarehe 05 Juni 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Zahor Kassim El- Kharousy Sera ya Taifa ya Uchumi wa Buluu ya Mwaka 2024 mara baada ya kuizindua wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Dodoma tarehe 05 Juni 2024.

Katika Maadhimisho hayo Sera ya Taifa ya Uchumi wa Buluu ya mwaka 2024 na Mkakati wa Utekelezaji wa Sera hiyo kwa kipindi cha mwaka 2024 – 2034 imezinduliwa. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni kuhuisha ardhi iliyoharibiwa, kuzuia kuenea kwa jangwa na kujenga ustahimilivu dhidi ya ukame.

Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mussa Zungu, Waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo,
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimkabidhi Kiongozi wa Machifu kutoka mkoani Mbeya Chifu Rocket Masoko Mwanshinga Sera ya Taifa ya Uchumi wa Buluu ya Mwaka 2024 mara baada ya kuizindua wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Dodoma tarehe 05 Juni 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akikabidhiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa zawadi ya Tuzo ya Mazingira kwa ajili ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutambua mchango wake katika uhifadhi mazingira na uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi ya kupikia kitaifa na kimataifa. Tuzo hiyo imetolewa wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Dodoma tarehe 05 Juni 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Mrindoko mfano wa hundi ya shilingi Bilioni 14.2 iliyotokana na biashara ya kaboni wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Dodoma tarehe 05 Juni 2024.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM John Mongela, Mwakilishi wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa Nchini Clara Makenya, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule, Mawaziri mbalimbali,

Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu, Wabunge, Viongozi wa Taasisi mbalimbali za Serikali na Binafsi,Viongozi wa dini, Viongozi wa Kimila,Mabalozi wa Mazingira pamoja na wananchi mbalimbali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news