Makamu wa Rais amwakilisha Rais Dkt.Samia mazishi ya Dkt.Saulos Chilima nchini Malawi

LILONGWE-Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amemwakilisha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Kitaifa ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Malawi Hayati Dkt. Saulos Klaus Chilima. Ibada ya Mazishi hayo imefanyika katika Uwanja wa Taifa wa Bingu uliopo Lilongwe nchini Malawi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kamuzu, Lilongwe nchini Malawi ambapo anatarajiwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Kitaifa ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Malawi Hayati Dkt. Saulos Chilima leo tarehe 16 Juni 2024.
Akitoa salamu za rambirambi, Makamu wa Rais amesema Tanzania inatoa salamu za pole na kuungana na waombolezaji wote walioguswa na msiba huo katika kipindi hiki kigumu.

Makamu wa Rais amesema Hayati Chilima alikuwa kiongozi imara, mwanamajumui wa kweli wa Afrika ambaye wakati wote alitanguliza mbele maslahi ya wananchi anaowaongoza na Afrika kwa ujumla.

Pia Makamu wa Rais amemtaja Hayati Chilima kama kiongozi aliyesimamia umoja, amani na usalama, mageuzi ya kiuchumi ya Malawi na utawala wa kidemokrasia nchini humo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akitoa salamu za rambirambi wakati wa Mazishi ya Kitaifa ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Malawi Hayati Dkt. Saulos Chilima katika Uwanja wa Taifa wa Bingu uliopo Lilongwe nchini Malawi leo tarehe 16 Juni 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akishiriki katika Ibada ya Mazishi ya Kitaifa ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Malawi Hayati Dkt. Saulos Chilima katika Uwanja wa Taifa wa Bingu uliopo Lilongwe nchini Malawi leo tarehe 16 Juni 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akishiriki katika Ibada ya Mazishi ya Kitaifa ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Malawi Hayati Dkt. Saulos Chilima katika Uwanja wa Taifa wa Bingu uliopo Lilongwe nchini Malawi leo tarehe 16 Juni 2024.

Makamu wa Rais amesema wananchi wa Malawi na Ukanda wote kwa ujumla wanapaswa kumuenzi Hayati Chilima kwa kuendeleza yale aliyosimamia na kuendelea kumuombea apumzike kwa amani.

Katika kushiriki Mazishi hayo ya Kitaifa Makamu wa Rais ameambatana na Waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe.Hamza Hassan Juma, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato pamoja na Balozi wa Tanzania Mhe. Agnes Kayola.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news