Makamu wa Rais Dkt.Mpango aifariji familia ya marehemu Tixon Nzunda

KILIMANJARO-Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema watumishi wa Umma wanapaswa kumuenzi aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro, marehemu Tixon Nzunda kwa kuwa waadilifu, wazalendo na kumtanguliza Mungu katika majukumu yao.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimfariji Bi. Grace Mgombela ambaye ni Mjane wa aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Marehemu Tixon Nzunda pamoja na familia yake mara baada ya kuwasili nyumbani kwa familia hiyo Moshi mkoani Kilimanjaro tarehe 19 Juni 2024.
Makamu wa Rais amesema hayo wakati akizungumza na waombolezaji alipowasili nyumbani kwa aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Marehemu Tixon Nzunda, Moshi mkoani Kilimanjaro.
Amesema, marehemu Nzunda alikuwa kiongozi na mtumishi wa umma muadilifu na makini katika nafasi mbalimbali alizowahi kuzitumikia serikalini.

Amesema, serikali imeguswa na msiba huo na inaungana na waombolezaji wote katika kipindi hiki kigumu.

Aidha, amewashukuru wananchi kwa kujitoa na kuwa pamoja na familia tangu ilipofikwa na msiba huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisali pamoja na familia ya aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Marehemu Tixon Nzunda mara baada ya kuwasili nyumbani kwa familia hiyo Moshi mkoani Kilimanjaro tarehe 19 Juni 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na waombolezaji mbalimbali mara baada ya kuwasili nyumbani kwa aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Marehemu Tixon Nzunda Moshi mkoani Kilimanjaro tarehe 19 Juni 2024.
Vilevile Makamu wa Rais amewasihi watanzania kuendelea kuishi vema kazini, kuishi vema na marafiki pamoja na majirani.

Amewaasa waombolezaji kupokea msiba huo kama ni mipango ya Mungu na kumuombea marehemu apumzike kwa amani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na waombolezaji mbalimbali mara baada ya kuwasili nyumbani kwa aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Marehemu Tixon Nzunda Moshi mkoani Kilimanjaro tarehe 19 Juni 2024.
Halikadhalika Makamu wa Rais ametoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu Alphonce Edson aliyekuwa dereva wa Marehemu Tixon Nzunda waliofariki pamoja katika ajali ya gari Wilaya ya Hai mkoani Kilimanajro tarehe 18 Juni 2024.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news