Mambo ya Ndani yakabidhiwa Kikombe na Cheti utoaji taarifa kwa umma

DAR-Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imekabidhiwa Kikombe na Cheti baada ya kuibuka mshindi wa pili katika utoaji wa taarifa kwa Umma katika kipindi cha mwaka 2023/2024. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imeibuka na ushindi huo wa pili kati ya Wizara Kumi Bora na kati ya Wizara 26 za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tuzo hizo zimekabidhiwa Juni 21,2024 na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye wakati akifunga Kikao Kazi cha 19 cha Maafisa Habari wa Serikali, katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news