Mamia wamiminika katika Kliniki ya Ardhi jijini Dodoma

DODOMA-Wananchi wa Jiji la Dodoma na viunga vyake wameendelea kujitokeza katika Kliniki ya Ardhi ili kutatuliwa migogoro ya ardhi inayowakabili.
Wananchi wakisubiri kupata huduma kwenye Kliniki ya Ardhi inayoendelea jijini Dodoma leo Mamia ya wananchi wamemiminika katika viwanja vya Ofisi za Halmashauri ya jiji la Dodoma kutatua madhila ya ardhi yanayowakabili ili watumie ardhi na muda wao kwa shughuli za kiuchumi kujiletea maendeleo.

Kamishna wa Ardhi, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Methew Nhonge amesema Watendaji wakuu wa Wizara pamoja na watendaji wa Ardhi mkoa wa Dodoma wapo katika eneo la Ofisi ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma kutoa huduma kwa wananchi wanaofika eneo hilo kupata huduma za ardhi.

Kwa kipindi cha siku mbili tangu Juni 3-4, 2024 jumla ya wanaanchi 996 wamefika katika viwanja hivyo na kupatiwa huduma kulingana na mahitaji yao.

Watendaji hao wamepiga kambi katika Ofisi hizo kwa lengo la kutekeleza agizo la Mhe. Jerry Silaa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi alilolitoa Bungeni Mei 27, 2024 la kuhamisha Masijala ya Ardhi kutoka jiji la Dodoma na kuzihamishia katika Ofisi za Wizara ili kutatua migogoro ya ardhi katika kituo kimoja jumuishi (One Stop Center).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news