Mara wapongezwa kwa ukusanyaji wa Maduhuli

MARA-Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo ameipongeza Ofisi ya Madini Mkoa wa Mara kwa ukusanyaji wa Maduhuli ya Serikali licha ya kukabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo hali ya mvua nyingi.
Mbibo ametoa pongezi hizo leo Juni 18, 2024 wakati wa ziara yake mkoani humo ambapo taarifa ya Afisa Madini Mkazi imebainisha kuwa jumla ya shilingi bilioni 111.3 zilikusanywa hadi kufikia Juni 14, 2024 sawa na asilimia 72.3 ya lengo la mwaka la kukusanya shilingi bilioni 153 katika Mwaka wa Fedha 2023/24.
Akizungumza katika kikao baina yake na watumishi wa ofisi hiyo, Mbibo amesisitiza kuzingatiwa kwa taratibu za utoaji leseni kama Sheria inavyotaka pamoja na kuwataka watumishi kuendeleza ushirikiano mzuri mahali pa kazi na kwa wadau wa sekta hiyo.

Pia, amewataka watumishi kutumia vizuri muda wa kazi, kuwa waadilifu ikiwemo kuepuka rushwa pamoja na kuhakikisha wanasuluhisha migogoro inayojitokeza kwa wachimbaji ili kuepusha hasara zinazoweza kujitokeza baadaye ikiwemo uharibifu wa mali na upotevu wa maisha ya watu.
Mkoa wa Mara umebarikiwa kuwa na aina mbalimbali za madini ambapo madini yanayopatikana mkoani humo ni pamoja na dhahabu, shaba, fedha, chuma, chokaa, soapstone na madini ya ujenzi. Madini yanayochimbwa kibiashara ni dhahabu, fedha na madini ujenzi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news