Mathias Canal aunga mkono juhudi za Mbunge Bashungwa,achangia shilingi milioni 1 za madawati Shule ya Msingi Kigasha

KAGERA-Kufuatia juhudi zinazofanywa na Mbunge wa Jimbo la Karagwe ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi,Mheshimiwa Innocent Bashungwa katika kuimarisha sekta ya elimu ikiwemo ujenzi wa shule mpya ya Msingi ya Kigasha, mwandishi wa habari Mathias Canal amechangia shilingi milioni 1 kwa ajili ya madawati.
Mathias amechangia madawati hayo mara baada ya kutembelea shule hiyo iliyopo katika Kata ya Rugu, Tarafa ya Nyaishozi akiwa katika kazi ya kutembelea miradi ya maendeleo ikiwa ni sehemu ya kujionea utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025.

Amesema kuwa, usimamizi wa ujenzi wa shule hiyo unaenda sambamba na serikali kupeleka walimu ambapo ametumia nafasi hiyo kumpongeza Waziri wa Elimu, Mhe. Prof Adolf Mkenda kwa kuweka kipaumbele katika shule hiyo ili kuhakikisha wanafunzi wa maeneo hayo wanapata elimu bora kama ilivyo katika maeneo mengine.
Kwa upande wake Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Karagwe,Ivo Ndisanye amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa kipaumbele katika sekta ya elimu ikiwemo ujenzi wa shule na upatikanaji wa walimu.

Pia kwa niaba ya Mbunge, Mhe.Innocent Bashungwa,katibu huyo ameahidi kuchangia shilingi milioni 3 kwa ajili ya upatikanaji wa madawati ili kuimarisha ufanisi wa kujifunza.
Ivo amewapongeza wazazi na walezi wa wanafunzi katika kijiji hicho, kwani kupitia nguvu za wanachi wameweza kujenga madarasa mawili ambayo mbunge alitoa mabati kwa ajili ya kupaua.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news