Mbeya Cement yatoa gawio la shilingi bilioni 3 serikalini

MBEYA-Baada ya miaka 10 bila matokeo chanya, Kiwanda cha Saruji Mbeya kinachojulikana kwa chapa ya Tembo kimetoa gawio la shilingi bilioni 3 kwa Serikali.
Hatua hiyo inafikiwa baada ya kiwanda hicho kutengeneza faida ya shilingi bilioni 161.3 katika kipindi cha mwaka 2023.
Tangu mwaka 2014, kiwanda hicho kinachomilikiwa kwa ubia kati ya Kampuni ya Amsons kutoka Holcim ya Uswisi yenye hisa asilimia 65,Serikali ya Tanzania kupitia Msajili wa Hazina yenye hisa asilimia 25.
Sambamba na Shirika la Taifa la Hifadhi za Jamii (NSSF) wenye hisa asilimia 10, hakijawahi kutoa gawio serikalini huku kikijiendesha kwa hasara.

Hata hivyo,mabadiliko hayo ni matokeo chanya ya 4Rs za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan zinazolenga kufanya mabadiliko katika uendeshaji wa mashirika ya umma nchini.
Kwenye uongozi wake, Rais Dkt. Samia anaamini katika kile kinachojulikana kama 4Rs ikiwa ni ufupisho wa maneno manne ya lugha ya Kiingereza; Reconcilation (Maridhiano), Resilience (Ustahamiliivu), Reforms (Mabadiliko) na Rebuidlding (Kujenga Upya).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news