Mbunge Yustina Rahhi kutinga Kiteto kesho kwa muendelezo wa Mafunzo ya Siku Tano ya Ujasiriamali

MANYARA-Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Manyara, Mheshimiwa Yustina Rahhi ameandaa mafunzo ya ujasiriamali ili kuwajengea uwezo wanawake na vijana wajasiriamali wa Mkoa wa Manyara.

Lengo likiwa ni kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan kuelekea uchumi wa kati.Mheshimiwa Rahhi amesema,  mafunzo hayo Kimkoa yameanzia Wilaya ya Mbulu toka Mei 20 hadi Juni 28,2024 yatakapomaliza mkoani humo.
Mbunge Rahhi amesema,walengwa wa mafunzo hayo ni wanawake waajasiriamali wote kuanzia ngazi za matawi hadi wilaya wakiwemo viongozi mbalimbali kama madiwani wa viti maalum, madiwani wa kata wanawake, na viongozi wa UWT ngazi ya matawi hadi wilaya.
"Kwa Wilaya ya Kiteto, mafunzo haya yatatolewa kuanzia Juni 24 hadi Juni 28, kuanzia saa mbili asubuhi na kumalizika saa nane mchana katika ukumbi wa Kauli Njema (TESHA)," amesema Mheshimiwa Rahhi.
Aidha, Mheshimiwa Rahhi ametaja mada mbalimbali zitakazofundishwa kwa wajasiriamali hao kuwa ni pamoja na Ufugaji kibiashara, Kilimo Biashara, Batiki aina zote, Sabuni aina zote, Keki Pili pili kali, Karanga, Tambi, Utafutaji wa masoko, na usimamizi wa Biashara.
Katika Wilaya ya Mbulu baada ya mafunzo, Mbunge Rahhi aliwezesha kutoa vifaranga 4000, Hanang' pia ametoa vifaranga 4000.

Aidha,baada ya mafunzo hayo Mbunge Rahhi atawezesha kutoa mtaji wa vifaranga vya kuku vipatavyo 4000 kwa washiiriki wote wa mafunzo ya ujasiriamali watakaokuwepo wilayani Kiteto.
Hata hivyo amewataka wanawake hao wajasiriamali kuhakikisha wanahudhuria mafunzo hayo kikamilifu ili kuweza kutoka hapo wakiwa na elimu nzuri na kubwa ya ujasiri na hatimaye waweze kujikwamua kiuchumi na na umaskini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news