DAR- Juni 15, 2024 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan ameteuliwa Thobias Makoba kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari-Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali.
Bw. Makoba anachukua nafasi ya Mobhare Matinyi ambaye amepangiwa majukumu mengine. Kabla ya Uteuzi huu Bw. Makoba alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika Ofisi ya Majili wa Hazina.
Kabla ya kujiunga na Ofisi ya Msajili wa Hazina, Bw. Makoba alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mwandamizi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Pamoja na kushiriki katika majukwaa mbalimbali ya Kimataifa ikiwemo UN, African Union, SADC, EAC, World Economic Forum na mengineyo, kwa vipindi mbalimbali aliwahi kuwa Katibu wa Mawaziri wawili wa Mambo ya Nje, hayati Bernard Membe na baadaye Balozi Dokta Augustine Mahiga kabla ya kwenda kuwa Kaimu Mkurugenzi Msaidizi katika Ofisi ya Mambo ya Nje Zanzibar.
Bw. Makoba ana Masters Degree in Security and Strategic Studies kutoka National Defence College-Tanzania, Post-Graduate Diploma in Economic Diplomacy kutoka Chuo Cha Diplomasia Kurasini na Degree ya kwanza ya Political Science and Sociology with majors in International Relations.
Tags
Habari
Idara ya Habari MAELEZO
Msemaji Mkuu wa Serikali
Ofisi ya Msajili wa Hazina
Thobias Makoba