Mhandisi Mativila aridhishwa na ujenzi wa barabara Morogoro,daraja la Lukuyu mkombozi kwa wakulima

MOROGORO-Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI anayesimamia Miundombinu,Mhandisi Rogatus Mativila ameridhishwa na ujenzi wa barabara ya kichangani iliopo manispaa ya Morogoro iliyogharimu zaidi shilingi milioni 400.Mhandisi Mativila ameyasema hayo leo Juni 19,2024 wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu ya barabara inayosimamiwa na Wakala ya Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA).
Amesema kwamba, kukamilika kwa barabara hiyo itaenda kufungua shughuli za kiuchumi kwa wakazi wa eneo hilo.

“Ni wakati sasa wa wakazi wa eneo hili kunufaika kupitia miundombinu ya Barabara ili kuweza kuwarahisishia mawasiliano na shughuli za usafirishaji.”

Hata hivyo Mhandisi Mativila amewataka TARURA manispaa ya Morogoro kumalizia kipande cha barabara ya mfungua kinywa kabla ya mvua hazijaanza kunyesha.

Wakati huo huo Mhandisi Mativila ameiagiza TARURA manispaa ya Morogoro kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa daraja la Lukuyu lililopo Kata ya Bigwa liwe limekamilika ifikapo Agosti mwaka huu ili kuwaondolea adha wananchi wa maeneo hayo kusafirisha mazao yao ikiwemo mboga mboga ,ndizi kwa kubeba kichwani.
Daraja la Lukuyu litagharimu kiasi cha shilingi milioni 70 na kikamilika kwa ujenzi wa daraja hilo linaenda kuwa mwarobaini kwa wakazi wa Kata ya Bigwa.

Kwa upande wake Meneja wa TARURA Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Emmanuel Ndyamukama amesema kuwa barabara ya kichangani ni miongoni mwa barabara ambazo zinaenda kuchochea manispaa ya Morogoro kuwa jiji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news