Miundombinu ya michezo itaendelea kuboreshwa-Waziri Mkuu

TABORA-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali inaendelea kutekeleza mpango wa kuboresha miundombinu ya michezo katika shule teule 56 nchini.
Amesema hadi kufikia Machi 2024 imeshapeleka shilingi billioni nne kwa ajili ya kuboresha miundombinu katika shule za sekondari 26 za amali.

Ameyasema hayo leo Jumamosi, Juni 8, 2024 alipofungua Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi na Sekondari Tanzania, Tabora. Amefungua mashindano hayo kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Aidha, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kumpongeza na kumshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwezesha na kuhamasisha ufundishaji wa michezo katika shule za Msingi na Sekondari nchini.

Waziri Mkuu amesema shule 10 zilizopelekewa fedha za maboresho ni za michezo na sanaa na ni miongoni mwa shule teule 56 za michezo.
Amesema,lengo la Serikali ni kuendelea kuboresha na kuweka mazingira mazuri ya michezo na sanaa nchini kwa ajili ya kuandaa wataalam na wanamichezo mahiri.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali inaamini kwenye uwekezaji katika michezo ya wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari kwani unasaidia kwenye maandalizi ya mchezaji kuwa mahiri na kufanya vizuri ndani na nje ya nchi.
“Hii ndio sababu ya uwepo wa mashindano haya ya michezo ya UMITASHUMTA na UMISSETA ambayo yanasaidia kuibua vipaji mbalimbali vya wanamichezo watakaoweza kucheza michezo mbalimbali kwa ngazi za kitaifa na kimataifa.

“Michezo ina manufaa makubwa katika maisha yetu. Kwanza kabisa, michezo husaidia afya ya mwili na akili, amani ya nafsi, kupata pesa na uongeza umaarufu.

“Kwa upande wa wazazi na walezi, hakikisheni na himizeni ushiriki wa watoto katika michezo au sanaa ili wasijitenge na fursa zinazopatikana katika dunia ya sasa.”
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI amesema kwa mwaka huu mashindano ya UMITASHUMTA yamehusisha wanamichezo 3188, na walimu na viongozi 805 kutoka Tanzania Bara na Visiwani.

Ameongeza kuwa,Mashindano ya UMISSETA yatahusisha wanamichezo 3360, na walimu na viongozi 900.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news